Andre Villas Boas atapoteza kiasi kinachokaribia £11million wakati atakapotangazwa kuwa kocha mpya wa Tottenham wiki ijayo.
Mreno huyo, 34, hakupokea fidia yote kwa pamoja ya kuvunjika kwa mataba
wake alipofukuzwa na Chelsea mwezi wa tatu mwaka huu, ikiwa ni miezi
nane tu tangu aliposainishwa mkataba wa miaka 3.
Badala yake, Chelsea walikubaliana na AVB kuendelea kumlipa msharaha
wake wa kawaida wa £100,000 kwa wiki mpaka pale atakapopata kazi mpya.
Mpaka sasa ameshapokea mshara wa miezi mitatu tangu kuanza mpaka mwishoni mwa mwezi huu.
Lakini ikiwa atakuwa kocha wa bosi wa White Hart Lane, Mmiliki wa
Chelsea Roman Abramovich ataachana na mpango wa kumlipa mshahara AVB, na
kocha huyo atapoteza mkwanja wa malipo ya miezi 25 iliyobaki yenye
thamani ya £10.8million.
Ripoti kutoka nchini Ureno zinasema kwamba mazungumzo kati ya AVB na Spurs yamekwamia kwenye suala la fedha.
|
No comments:
Post a Comment