Uongozi wa klabu ya Azam umesema tayari imepokea
maombi ya makocha 12 wanaowania nafasi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo.Maombi
ya makocha hayo yanatokana na uamuzi wa hivi karibuni uliotangazwa na uongozi wa
klabu ya Azam wa kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Stewart
Hall.
Baada ya kutangazwa kuondolewa kikosini, klabu hiyo ilimtangaza
kocha wa muda, Vivek Nagul raia wa India atakayesaidiana na Kalli
Ongala.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema kuwa miongoni mwa maombi
yaliyopokelewa ni ya makocha wazawa na mengine ni ya makocha kutoka nje ya
nchi.
"Kikubwa ni kwamba tumepokea maombi ya makocha 12 mpaka sasa
miongoni mwao ni wazawa na wengine kutoka nje ya nchi,".alisema
Mohamed.
Hata hivyo, Mohamed hakuwa tayari kutaja majina ya makocha wala
nchi wanazotoka kwa madai kwamba bado wanafanya upembuzi yakinifu na muda si
mrefu wataweka bayana.
Aliongeza kuwa, vigezo vitakavyotumika katika
kumpata kocha wao mpya ni rekodi zake katika kufundisha soka na si
vinginevyo.
Wakati huu huo, Mohamed amekanusha taarifa zilizoripotiwa na
baadhi ya vyombo vya habari kuwa klabu yake imemtimua Hall baada ya kumpanga
Winga Mrisho Ngasa katika pambano dhidi ya Yanga.
"Niweke wazi kwamba
uongozi wangu unafanya kazi kwa kuzingatia ushauri wa benchi la ufundi ,hakuna
tuhuma zozote zilizoletwa kwetu zinazomhusu Ngassa, sasa kwanini tumfukuze
kocha, huo ni uzushi tu.
Kukanusha
huku kwa Azam kwamba walimfukuza Stewart kunakuja siku mbili baada ya baadhi ya
vyombo vya habari kuripoti kwambakocha huyo alitimuliwa baada ya kumpanga Ngassa
kwenye fainali japokuwa likatazwa kufanya hivyo na uongozi wa AZAM FC.
|
No comments:
Post a Comment