ug 1 2012 Jumatano jioni
kilichoandikwa kwenye website ya club ya soka ya Azam Fc kuhusu mchezaji
wao Mrisho Ngasa kuuzwa ghafla ni hiki, “Biashara na Mjadala wa Mrisho
Ngasa umefungwa leo mchana saa tisa kasorobo baada ya Simba SC
kuizidi nguvu Yanga na kutoa shilingi milioni 25, ofa ya Yanga iliiishia
milioni 20″
Azam FC inamtakia kila la heri na mafanikio mema Mrisho Ngasa kwenye klabu yake mpya ya Simba.
Hayo yote ni maelezo
yaliyotolewa kwenye website ya Azam Fc ambapo mpango wa kumuuza
haukuwepo kabisa, umekuja ghafla baada ya kumalizika kwa mashindano ya
Kagame Cup.
kama bado unashangaa kwa nini
Ngasa ameuzwa mapema hivi nataka kukwambia kwamba juzi yani Jumanne july
31 kwenye website ya Azam kuliandikwa hivi “Hadi hivi sasa Ofa ya Simba
ni shilingi Milioni 25 na Yanga ni Milioni 20, kutokana na hilo Simba
wapo kwenye nafasi kubwa ya kumnyakua Mrisho Ngasa. Kesho ni siku ya
Mwisho. Ingawa tungependa kumuuza Mrisho Ngasa Yanga lakini tutampeleka
kwa timu iliyotoa ofa nzuri zaidi”
Kwenye sentensi nyingine
wakaandika “Lengo la Azam FC lilikuwa ni kumpeleka Mrisho kwenye timu
ambayo atacheza kwa raha na amani kutokana na yeye kuivaa na
kuibusu Jezi ya Yanga siku ambayo Azam FC haikuwa na mchezo na Yanga…
Azam FC inaamini kuwa Yanga ilikuwa Sehemu sahihi kwa Mrisho,
lakini uongozi wa Yanga umeonekana kutokuwa na haja na Mrisho na ndiyo
maana umeonekana kukataa kutoa ofa ya maana, Kutokana na sababu hizo
Azam FC italazimika kumuuza Mrisho Ngasa Simba kwani hatuhitaji kuwa
na mchezaji ambaye anafanya vitendo vya kuidharau brand ya Azam FC
ambayo tunajaribu kuijenga” – Azam Fc
Imefahamika kwamba kitendo cha
Ngasa kuivaa na kuibusu jezi ya Yanga ndio kitu pekee kilichowakasirisha
maboss wa club hiyo na kuamua kumuuza mchezaji huyo ambapo Azam walitoa
taarifa za kumuuza mchezaji huyo July 30 2012 na kuandika kwamba “Klabu
ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa milango iko wazi kwa klabu
yoyote kumnunu mchezaji Mrisho Ngassa kwa gharama ya $ 50,0000″
“Azam FC imefikia hatua hiyo
baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo na
badala yake kuipenda klabu aliyotoka ya Yanga hivyo uongozi wa klabu
unapokea maombi kwa klabu yoyote inayomuhitaji, Ngassa
anauzwa siku chache baada ya kukubali kuvaa jezi ya Yanga na kuibusu
logo ya timu hiyo, baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali kati
ya Azam FC na AS Vita Club ya Congo DRC katika mashindano ya Kombe la
Kagame yaliyomalizika Julai 28 mwaka huu” – Azam Fc |
No comments:
Post a Comment