Baada ya jaribio lake la kutaka
kuendelea na kibarua chake kwenye timu ya Al Wasl, Diego Maradona ametoa
kali nyingine baada ya kusema aligundua ametimuliwa kwenye klabu hiyo
kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
Maradona, 51, alitimuliwa
na Al Wasl mapema mwezi huu baada ya kuwa na msimu mbaya wa kwanza
kwenye mkataba wake wa miaka miwili aliosaini mwezi May 2011.
Sasa
baada ya wiki iliyopita kukataa uamuzi wa kutimuliwa na kusisitiza
atakutana na viongozi wa timu hiyo ya Dubai na kumaliza tofauti zao
zilizopelekea kutimuliwa, jana maradona ameibuka na kuiambia radio
station ya Perros de la Calle kwamba hakutaarifiwa rasmi uamuzi wa
kutimuliwa mpaka pale alipokuja kugundua kupitia mtandao wa kijamii wa
Twitter.
"Ukweli ni kwamba niligundua kuota nyasi kibarua changu
kupitia Twitter sio jambo zuri. Nilikuwa nafanya kazi mpaka pale
walipoamua kufanya mabadiliko. Klabu ni mali yao na siwezi kusema
chochote kwa kuwa wao ndio wana haki ya kufanya chochote pamoja na
kuchagua kocha wao."
Mpaka wiki iliyop[ita Maradona hakuwa
amepokea taarifa rasmi ya klabu ya kumtimua kazi, mpaka pale mwenyekiti
wa Al Wasl Mohamed Bin Dukhan waliwasiliana na Maradona kupitia ubalozi
wa Argentina kwa msaada wa mtafsiri lugha wa kihispaniola. |
No comments:
Post a Comment