Mapema mwaka jana, Manchester City,
inayomilikiwa na mmoja ya wanafamilia wa familia ya kifalme ya Abu
Dhabi, iliingia mkataba wa udhamini ulio mnono zaidi katika historia ya
soka na Etihad Airways, ambayo inamilikiwa na familia ya kifalme ya Abu
Dhabi. Hii ilionekana kama ni janja ya City kuweza kuepeukana na
matatizo ambayo wangeweza kukutana nayo dhidi ya sheria ya Financial
Fair Play, ambayo inahitaji vilabu kutumia fedha kwa kadri inavyoingiza
tu na sio kutoka mfukoni kwa mtu/watu fulani, rafiki au ndugu/familia.
Baada ya City kufanya hivyo, sasa watumiaji wengine wakubwa wa EPL,
klabu ya Chelsea nayo imesaini mkataba wa wenye thamani kubwa na kampuni
ya Gazprom Energy.
Gazprom, ni kampuni kubwa ya nishati nchini Urusi, imesaini mkataba wa
miaka mitatu huku thamani halisi ya deal hilo ikiwa imefichwa na pande
zote mbili. Hii sio mara ya kwanza kwa mmiliki wa Chelsea kufanya
biashara na Gazprom .
Gazeti la Telegraph la Uingereza linaeleza:
"Sheria ya UEFA inawalazimisha vilabu kuacha kukubali dili za udhamini
kutoka kwa watu/kampuni zenye mahusiano nazo. Mmiliki wa Chelsea Roman
Abramovich, aliuza hisa zake kwenye kampuni ya mafuta ya Sibneft kwenda
Gazprom kwa £8.4 billion mwaka 2005 na Uefa na sheria zake zinakataza
uhusiano kama huu kwenye - ambapo mmiliki wa klabu anakuwa na uhusiano
na kampuni inayotoa udhamini kwa klabu."
Lakini Manchester City wameweza kupita na dili lao la rekodi ya dunia na
Etihad, basi na mkataba wa Chelsea na Gazprom itabidi uvuke vikwazo vya
UEFA - kwa kuwa Abramovich alishauza hisa zake za kampuni yake ya
zamani kwa mdhamini mpya wa Chelsea kwa hiyo anaweza kusema hana nguvu
yoyote katika kukamilika kwa udhamini huo wa Chelsea.
Kwa maana hiyo Chelsea na Manchester City wataendelea kutanua misuli ya
fedha kwenye soko la usajili pamoja na Platini kuleta sheria yake ya
Financial Fair Play. |
No comments:
Post a Comment