Wakiwa
wamekasirishwa na kuuzwa kwa Thiago Silva na Zlatan Ibrahimovic kwenda PSG,
kundi la mashabiki wa AC Milan walielezea hisia zao za kusikitikishwa na kitendo
hicho kwa niaba ya mashabiki wenzao walifanya kituko kikubwa mbele ya ofisi kuu
za klabu hiyo.
Kundi hilo la mashabiki lilifanya kitendo cha kuashiria
mazishi kwa kuweka kadi ya mazishi, mishumaa na maua mbele ya jengo la ofisi za
AC Milan, wakimaanisha klabu hiyo inakufa baada ya kuwauza wachezaji wake bora
wawili. Pia baada ya kufanya kitendo hicho mashabiki hao walifungua kesi dhidi
ya klabu hiyo kwa madai ya kutangaziwa vitu vya uongo.
Wakati huo huo, klabu imeamua kutoa ofa ya kuwarudishia
fedha zao mashabiki walionunua tiketi za msimu waliokasirishwa na kuuzwa kwa
Ibra na Silva.
"Uamuzi wa kuwarudishia fedha zao wanunuzi wa tiketi za
msimu, hauna uhusiano wowote na kesi tuliyofunguliwa," alisisitiza mkurugenzi
Leandro Cantamessa.
"Hii tumefanya kwa wale
ambao hawakuwa na furaha, hatuna ulazima wa kuwachezesha au kuwa na wachezaji
ambao wanunuzi wa tiketi za msimu wanawataka." |
No comments:
Post a Comment