Fainali ya kombe la Urafiki (ujirani
mwema) litawakutanisha mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara Simba SC
dhidi ya mabingwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC.
Simba SC na Azam FC zote za Tanzania Bara zimetinga hatua hiyo ya
fainali baada ya kuzifunga Zanzibar All Stars na Falcon, hii leo katika
michezo ya nusu fainali ya kombe hilo, ambalo michezo yake huchezwa
katika uwanja wa Amani.
Azam FC walikuwa wa mwanzo kukata tiketi ya fainali, baada ya kuwachapa
Falcon magoli 2-0. Shukran zimuendee mshambuliaji wa Ivory coast Kipre
Tchetche aliyefunga magoli yote mawili.
Kipre Herman Tcheche alifunga bao la kwanza dakika ya 67, akiunganisha
krosi ya Hamisi Mcha wakati bao la pili, alifunga kwa penalti, dakika ya
77, baada ya Samir Haji Nuhu kuangushwa kwenye eneo la hatari na Samir
Said dakika ya 77.
Wakati Azam wakitoa dozi hiyo Simba SC wao wameichapa goli 1-0 Zanzibar
All Stars. Goli hilo pekee la Simba limefungwa na Kanu Mbiavanga.
Fainali ya Urafiki Cup itachezwa julai 11 siku ya jumatano katika uwanja wa Amani Zanzibar |
No comments:
Post a Comment