Klabu ya bingwa
ya Tanzania bara Simba Sports Club leo imetupa karata nyingine kwenye
michuano ya Urafiki inayofanyika huko Zanzibar kwa kupepetena na
washindi wa pili wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita klabu ya Azam.
Matokeo
kwenye mchezo huo wa pili wa michunao hiyo yameishia kuwa sare ya 1-1.
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lilowekwa kimiani na
mshambuliaji wake mpya Danny Mrwanda katika dakika ya 35, kabla ya Azama
hawajasawazisha kupitia kwa mchezaji wao mpya kutoka Kenya George
Odhiambo 'Blackberry' sekunde kadhaa kabla ya filimbi ya mapumziko
kupulizwa.
Azam walicheza pungufu kwa takribani dakika 35 baada ya kiungo wao Abdulhalim Humud kupewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 52.
Simba
sasa inaongoza kwenye kundi lake kwa pointi nne, mabao matatu ya
kufunga na mawili ya kufungwa, wakati Azam FC ni ya pili kwa pointi zake
mbili.
|
No comments:
Post a Comment