Chelsea imedhibitisha kuwa
imekubaliana na mshambulizi wa Atletico Madrid na Uhispania Diego
Costa sasa atashuka Stamford bridge msimu ujao.
Klabu hiyo ya London imedhibitisha kuwa
imeafikiana na Atletico Madrid kutumia kipengee cha kumnunua mshambulizi
huyo mwenye umri wa miaka 25 .
Hadi kufikia sasa haijadhibitisha
gharama yake itakuwa kiasi gani lakini wandani katika klabu hiyo
wanasema Costa huenda akaigharimu The Blues takriban dola milioni 55m
Mzaliwa huyo wa Brazil aliifungia Atletico mabao
35 msimu uliopita na kuisadia timu hiyo kufuzu kwa fainali ya kombe la
mabingwa barani ulaya walikoshindwa na mahasimu wao wa jadi Real Madrid .
Kocha wa wa the Blues Jose mourinho amekuwa
akiimarisha kikosi chake kwa kusajili nguvu mpya na pia kuna dukuduku
kuwa wachezaji wazoefu wa Chelsea Ashley Cole na Frank Lampard huenda
wakaondoka Stamford Bridge.
Mwezi uliopita Mourinho alimsajili aliyekuwa
kiungo wa Arsenal Cesc Fabregas huku kandarasi ya kipa Mark Schwarzer
ikiongezwa muda
No comments:
Post a Comment