PSI

PSI

Monday, January 19, 2015


 HISTORIA YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA (AFCON)

10407052_549055771898556_6171758218744726883_n
        kwa sasa mashindano haya ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili ni ya tatu kwa kufuatiliwa baada ya kombe na dunia na michuano ya mataifa ya Ulaya (EURO). katika ushiriki timu zimekua zikiongezeka ambapo kwa sasa timu 16 hushiriki tangu 1996
kwa mara ya kwanza mashindano haya yalifanyika kunako mwaka 1957 huku ikishirikisha matatifa manne pekee ya Misri, Sudan, Ethiopia na Afrika ya Kusini. Hata hivyo Afrika ya kusini iliondolewa baadaye kufuatia madai ya ubaguzi wa rangi nchini humo. Hata hivyo kiuhalisia taifa hilo liliondolewa baada ya kushindwa kupeleka timu yenye matabaka ya weusi na weupe. 
Hii ilisababisha Ethiopia kufuzu moja kwa moja katika hatua ya Fainali ambayo ilimalizika kwa kufungwa na Misri ambao waliibuka washindi wa michuano hiyo baada ya kushinda 4-0. Mechi hiyo ilifanyika mnamo jumamosi ya tarehe 16 Februari 1957 huko Khartoum, Sudan.
kisha mnamo mwaka 1962, michuano hiyo iligawanywa katika hatua mbili. Hatua ya kufuzu na ile ya fainali. Katika hatua ya awali michezo hiyo ilihusishsa mechi za mtoano kwa kucheza nyumbani na ugenini.
 mnamo 1992, ulifanyika uboreshaji wa hatua hiyo ya kufuzu ambapo timu zilipangwa katika hatua hiyo baada ya kupitia mchujo. 
Idadi ya timu shiriki iliongezeka toka timu nane (8) katika mwaka 1986 mpaka kumi na mbili (12).
ilipofika 1996, idadi ya timu shiriki iliongezeka mpaka kufikia 16 ambapo pia Afrika ya kusini ilishuhudiwa ikirejeshwa kunako kinyanga’anyiro hicho. Kilichovutia zaidi ni wao ndio walioandaa michuano husika.
Katika hatua ya fainali hizo timu kumi na sita zilizofuzu ziligawanywa katika makundi manne ya timu nne nne. Washindi wawili wa mwanzo toka kila kundi walifuzu kwa hatua ya robo fainali kisha nne kati ya hizo zikacheza nusu fainali na baadaye kupatikana wababe wawili ambao walipambana kupata bingwa wa michuano hiyo. Ikumbukwe kuwa bingwa wa michuano husika huwakilishwa bara la Afrika kunako kombe la Mabara.
Orodha ya washindi toka kuanza kwa michuano hiyo ni kama ifuatavyo 
Mwaka       Timu                      Fainali
1957           Misri                  
1959         Misri                  
1962         Ethiopia              
1963         Ghana                 
1965         Ghana                 
1968         Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (Zaire)
1970         Sudan
1972         Kongo (Brazzaville)
1974         Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo (Zaire)
1976         Morocco
1978         Ghana
1980         Nigeria
1982         Ghana
1984         Kameruni
1986         Misri
1988         Kameruni
1990         Algeria
1992         Côte d’Ivoire (Ivory Coast)
1994         Nigeria
1996         Afrika Kusini
1998         Misri
2000         Kameruni
2002         Kameruni
2004         Tunisia
2006         Misri
2008         Misri
2010         Misri
2012         Zambia
2013         Nigeria
2015          ?

Kumi bora ya wafungaji wa muda wote
1 . Samuel Eto’o Fils (Cameroon); (4) Ghana/Nigeria 2000; (1)Tunisia2004; (5)Egypt 2006
(5)Ghana 2008); (2)Angola 2010…Jumla 17
  1. Laurent Pokou (Côte d’Ivoire); (6)Ethiopia 1968; (8)Sudan 1970…Jumla 14
  2. Rashidi Yekini (Nigeria); (1)Morocco 1988; (3)Algeria 1990; (4)Senegal 1992; (5)Tunisia 1994…Jumla 13
  3. Hassan El Chazli (Misri) (6)Ghana 1963; (5)Sudan 1970; (1)Egypt 1974…Jumla 12
  4. Hossam Hassan (Misri) ;(7)Burkina Faso 1998, (3)Ghana/Nigeria 2000; (1)Egypt 2006…Jumla 11
  5. Patrick Mboma (Cameroon) (4)Ghana/Nigeria 2000; (3)Mali 2002; (4)Tunisia 2004….Jumla 11 7. Francileudo Dos Santos (Tunisia); (4) Tunisia 2004; (4)Egypt 2006, (2) Ghana 2008..Jumla 10
    8. Joël Tiehi (Côte d’Ivoire) (1)Senegal 1992; (4)Tunisia 1994; (1)South Africa 1996; (4)Burkina Faso 1998…Jumla 10
  6. Mulamba N’Daye (DR Congo); (9)Egypt 1974; (1)Ethiopia 1976; …Jumla 10
  7. Kalusha Bwalya (Zambia) (1)Egypt 1986; (1)Senegal 1992; (1)Tunisia 1994; (5)South Africa 1996; (1)Burkina Faso 1998; (1)Ghana/Nigeria 2000 Jumla 10
    10
REKODI NYINGINE MUHIMU
Mchezaji aliyewahi kufunga goli 5 mechi moja –
Laurent Pokou (Côte d’Ivoire) huko Sudan mwaka 1970 katika mechi baina ya Côte d’Ivoire/Ethiopia 6-1
Mchezaji aliyewahi kufunga goli 4 mechi moja
El Diba (Misri) huko Sudan mwaka 1957 katika mechi baina ya Egypt / Ethiopia 4-0
El Chazli (Misri) huko Ghana mwaka 1963 mchi baina ya Egypt / Nigeria 6-3
McCarthy (Afrika Kusini) huko B. Faso 1998 mechi baina ya Afrika Kusini/Namibia 4-1
Mchezaji aliyewahi kufunga goli 3 mechi moja
El Gohri (Misri) nyumbani Misri 1959 pambano baina ya Misri/Ethiopia 4-0
Manglé (Côte d’Ivoire) huko Tunisia 1965 mechi baina ya Côted’Ivoire/DRCongo 3-0
Lalmas (Algeria) huko Ethiopia 1968 mechi baina ya Algeria/Uganda 4-0
El Chazli (misri) huko Sudan 1970 mechi baina ya Misri/Côte d’Ivoire 3-1
Kaolo (Togo) huko Cameroon 1972 pambano baina ya Togo/Mali 3-3
Tiehi (Côte d’Ivoire) huko Tunisia 1994 pambano baina ya Côte d’Ivoire/S. Leone 4-0
Kalusha (Zambia) huko Afrika Kusini 1996 mechi baina ya Zambia/Sierra Leone 4-0
Hassan (Misri) huko B. Faso 1998 pambano baina ya Misri/Zambia 4-0
Santos (Tunisia) huko Misri 2006 pambano baina ya Tunisia/Zambia 4-1
Eto’o (Cameroon) huko Misri 2006 pambano kati ya Cameroon/Angola 3-1

ORODHA YA WAFUNGAJI BORA
Sudan 1957 El Diba Egypt 5
Egypt 1959 El Gohary Egypt 3
Ethiopia 1962 Badawi Egypt 3 & Menguistou Ethiopia 3
GHANA 1963 El Chazli Egypt 6
Tunisia 1965 Kofi Ghana 3; Acheampong Ghana 3;  Mangle Cote d’Ivoire 3
Ethiopia 1968 Pokou Cote d’Ivoire 6
Sudan 1970 Pokou Cote d’Ivoire 8, El Chazli Egypt 5
Cameroon 1972 Keita Mali 5 M’Bono Congo 4 Kaolo Togo 4
Egypt 1974; Ndaye Zaire 9, Abugreisha Egypt 4
Ethiopia 1976; Njo Léa Guinea 4 Faras Morocco 3 Gagarine Sudan 3
ZILIZOSHIRIKI MARA NYINGI ZAIDI
Egypt  (15)
Cote d’Ivoire  (10)
NYINGINE
  • Mara 11 wenyeji wameibuka mabingwa Egypt
    (1959, 1986, 2006), Ethiopia (1962), Ghana (1963 and 1978), Sudan
    (1970), Nigeria (1980), Algeria (1990), South Africa (1996) and Tunisia
    (2004).
  • mara 5 mabingwa wametetea mataji yao
Misri 1959 baada ya kutwaa 1957 kisha 2006-2008.
Ghana won it 1963 na 1965
Kameruni 2000 na 2002.

  • Ghana imecheza fainali 4 mfululizo kati ya 1963 na 1970,
Came roon imecheza mara tatu mfululizo (1984,
1986, 1988)

  • Misri nayo mara tatu, mara 2 (1957, 1959, 1962, na kisha 2006, 2008, 2010).
    goli la 1000 la michuano lilifungwa naye Augustine ‘Jay-Jay’ Okocha (2004)
Jumla ya mabao 1431 yamefungwa katika michezo 574 sawa na wastani wa goli2.60 kwa mechi  
  • Aliyeshiriki na umri mkubwa zaidi Hossam Hassan (Egypt): miaka 39 miezi 5 siku 24
  • Aliyeshiriki na umri mdogo zaidi Chiva Star Nzighou (Gabon): miaka 16 miezi miwil na siku 30 mwaka (2000)

No comments: