PSI

PSI

Thursday, June 28, 2012

Nasri aomba radhi vyombo vya habari

PARIS, Ufaransa
KIUNGO wa Ufaransa, Samir Nasri ameomba radhi waandishi wa habari kutokana na matamshi yake aliyoyatoa baada ya timu yake kutolewa katika Fainali za Euro 2012 kwa kufungwa na Hispania.

Nasri alishambuliwa na vyombo vya habari baada ya kuwatolea kauli chafu hasa baada ya timu yake kutolewa na Hispania kwa mabao 2-0.

"Naamini mashabiki na watu wengine walishangazwa na matamshi yangu, lakini yote ni hasira za kufungwa, naomba radhi," Nasri aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter.

"Naipenda Ufaransa, soka na pia nawapenda mashabiki wote."

Nasri, anayeichezea Manchester City, hakuwaomba radhi mashabiki mara baada ya matamshi yake: "Naweza kusema ni suala binafsi kati yangu na waandishi wa habari. Nitazungumza zaidi siku itakapowadia."

Kocha wa Ufaransa, Laurent Blanc alisema tabia ya Nasri haikumfurahisha yeye pamoja na wachezaji wengine.

"Lilikuwa tatizo kweli kati ya Samir na waandishi wa habari," Blanc aliiambia televisheni ya Ufaransa.


No comments: