Hatimaye mchezaji wa Bolton Fabrice Muamba ametangaza kuachana na soka leo hii kutokana na ushauri wa daktari.
Mchezaji
huyo mwenye asili ya Congo, alipata mshtuko wa moyo wakati wa mechi ya
FA Cup dhidi ya Tottenham, amesema ana uchungu mkubwa kuachana na
kucheza soka lakini hana budi zaidi ya kuweka mbele afya yake.
Muamba
ameishukuru sana timu ya madaktari kwa kuokoa maisha yake na ameshukuru
kwa maombi na sapoti kubwa aliyoipata kutoka kwa wapenzi wote wa soka
duniani.
Moyo wa Muamba ulisimama kwa saa 78 baada ya kudondoka
kwenye dimba la White Hart Lane baada ya kupatwa mshtuko wa moyo hali
iliyopelekea kufanyiwa matibabu na kuweza kuokoa maisha yake.
Alikaa
mwezi mzima Hosptali lakini aliwashangaza madaktari kwa jinsi
alivyopata nafuu kwa haraka huku akisistiza anataka urudi kwenye dimba
aendelee kucheza soka.
Kiungo huyo wa Bolton na England alienda
mpaka nchini Ubelgiji wiki iliyopita kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji
mdogo ili kuweza kuwa fiti kwa ajili kurudi uwanjani. |
No comments:
Post a Comment