PSI

PSI

Friday, August 24, 2012

JOHN BOCCO ANAHITAJI MAOMBI

MSHAMBULIAJI wa Azam FC, John Bocco, jana Alhamisi alitarajiwa kumaliza rasmi majaribio ya wiki mbili ya kuwania kusajiliwa na klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini.
Bocco ambaye alionyesha kiwango kizuri kwenye michuano ya Kombe la Kagame mwezi uliopita, aliitwa na klabu hiyo kwa ajili ya majaribio na kutimka Agosti 11, mwaka huu.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd alisema mpaka sasa bado wanasubiri majibu kutoka katika klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Alisema nafasi hiyo ilianza kugombewa na wachezaji tisa, wakachujwa wakabaki wanne akiwemo Bocco, ambapo amesema kuwa anayetakiwa ni mmoja. “Bado tunasubiri majibu, nafikiri akisharudi ndiyo tutajua,

No comments: