Timu ya Taifa ya Spain
imeendelea kukalia kiti cha uongozi wa ubora wa soka kwa mujibu wa
viwango vya FIFA. Mabingwa ha wa dunia na ulaya wameshikilia uongozi huo
wakiwa na pointi 1605, nafasi ya pili imekamatwa na Ujerumani, England
wameendelea kupanda ubora kwenye rank hizo za FIFA bada ya mwezi
uliopita kushika nafasi ya nne.
Brazil mabingwa wa mara tano
wa dunia wameendelea kuweka rekodi, baada ya kushika nafasi ya chini
zaidi katika historia yake, wakikamata nafasi 13, ikiwa ni mara ya
kwanza kushuka kwa namana hiyo.
Ivory coast ndio pekee ya
kiafrika kuwemo ndani ya 20 bora, wakishika nafasi ya 16. Timu ya taifa
ya Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 127 mpaka 128. |
No comments:
Post a Comment