Hii ni mara ya kwanza msimu huu kwa Arsenal kushindwa ikichezea uwanja wa nyumbani.
Nahodha wa Chelsea, John Terry, aliweza
kucheza katika mechi hiyo, huku akiwa bado anawaza kama atakata rufaa au
la, baada ya chama cha soka cha England cha FA, kumpiga marufuku ya
mechi 4, na kumtoza faini ya pauni 220,000, kwa kumpata na hatia ya
kutumia matamshi ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mchezaji wa QPR, Anton
Ferdinand.
Ushindi wa Chelsea ulipatikana kupitia bado
la mapema la Fernando Torres, ambaye aliweza kunyemelea nyuma ya Laurent
Koscielny, na kuusindikiza mkwaju wa free-kick kutoka kwa Juan Mata.
Gervinho aliweza kuisawazishia Arsenal kabla
ya kipindi cha kwanza kumalizika, lakini vijana wa Roberto Di Matteo
walitwaa pointi zao tatu katika kipindi cha pili, wakati mpira wa free-kick
kutoka kwa Mata uliweza kumgusa kidogo tu Koscielny na kukifanya
kibarua cha kipa wa Arsenal, Vito Mannone, kutoweza kuufikia mpira huo.
Mechi hii ni kipimo kizuri kwa meneja wa
Arsenal, Arsene Wenger, kuipima timu yake, na kudadisi ikiwa ina uwezo
wa kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Premier msimu huu.
|
No comments:
Post a Comment