Baada juzi kuiomba serikali kuwaondoa
viongozi wote wa shirikisho la soka la Senegal akiwalaumu kutokana
vurugu zilijitokeza kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast, leo hii mchezaji
mtukutu El
Hadji-Diouf amezungumza tena, na muda huu ametoa tuhuma kali dhidi ya
nahodha wake wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard. Katika mahojiano L’Equipe, mshambuliaji
wa Leeds alizungumzia kazi yake ya soka na tabia yake yake
isiyoridhisha, lakini zilikuwa kauli zake dhidi ya Gerrard ndizo
zilizoleta utamu wa mahojiano yake. Maneno ambayo kiukweli yalikuwa
yanalenga kujibu mapigo ya Gerrard aliyemuandika vibaya kwenye kitabu
chake kwa kumuita msenegali huyo Panya.
“Maneno ya Steven Gerrard? Ni wivu
tu. Nilikuwa ndio mchezaji muhimu zaidi kwa kipindi kile, na kila mtu
alikuwa akiniangalia mimi. Nilikuwa naisadia sana timu yangu ya taifa na
nilifanikiwa mpaka kuipeleka katika robo fainali kwenye World Cup 2002.
“Nilikuwa kwenye listi ya wachezaji
bora 100 wa karn waliotajwa na Pele na Gerrard hakuwemo. Namheshimu kama
mcheza soka, lakini hakuna mchezaji mbinafsi kama yeye. Alikuwa yupo
radhi Liverpool ifungwe lakini yeye afunge bao.
”Hajali kuhusu kitu chochote wala mtu yoyote. Nimeongea na magwiji wa Liverpool na wote wanachukizwa na tabia zake."
|
No comments:
Post a Comment