![]() |
| Ni vigumu sana kwa wachezaji makinda
kuweza kuwa na muda mrefu kwenye soka kwa miaka ya sasa hasa wanapokuwa
kwenye klabu kubwa kama Barcelona, mahala ambapo kuna presha kubwa na
nafasi hazijitoshelezi. Hivyo kuna wengine wanaamua kutafuta njia
mbadala ya kuingiza kipato popote wanapoweza. Na kijana mwenye umri wa
miaka 21 anayeicheza Barca ametuhumiwa kuiba pochi ya dereva taxi akiwa
njiani kwenda uwanja wa ndege kujiunga na wenzake wa kikosi cha Spain
cha under 21. Kutoka Marca: Dereva Taxi anaelezea kwamba akiwa anawaendesha mchezaji Montoya, na wachezaji wenzake Cristian Tello na Gerard Deulofeu, pamoja na Daktari Jorge, aliweka pochi yake katika siti ya mbele alipokaa Montoya na ghafla ya ikapotea.Kwa mujibu wa dereva, pochi hiyo ilikuwa na kiasi cha €230 na kadi ya hosptali ya mwanae wa kike. Montoya alijitetea kupitia mtandao wa Twitter, akisema tuhuma hizo ni za uongo na baadae akatoa taarifa rasmi ya aya tano kwa waandishi wa habari. |
PSI
Saturday, October 27, 2012
MCHEZAJI WA BARCELONA MPIGAJI: ATUHUMIWA KUIBA POCHI YA DEREVA TAXI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment