PSI

PSI

Tuesday, November 6, 2012

CESC FABREGAS NA TUHUMA ZA KUVUNJA NDOA YA WATU

Cesc Fabregas na girlfriend Daniella Semaan wamekuwa kwenye mapenzi mazito katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita. Walionekana wakila raha hivi karibuni wakati wa kipindi cha kiangazi huko Italy - lakini sasa kidudu mtu kimeanza kuingia kwenye mapenzi yao.

Aliyekuwa mume wa mchumba wake Fabregas, Millionea Elie Taktouk amejitokeza na kusema kwamba ulikuwa ndio wakati huo wa mapumziko ya kiangazi alipogundua mkewe anamsaliti - wakati wakiwa wanajaribu kupata mtoto wa tatu.


Millionea huyo amekuwa akizungumzia maumivu aliyoyapata juu ya usaliti wa mkewe aliyekuwa akiufanya na mchezaji wa Barcelona mwenye miaka 25

Akiongea na The Sun, Mfanyabiashara huyo alisema kwamba aligundua juu ya usaliti wa mkewe na nahodha huyo wa zamani wa Arsenal alipoona picha za wawili hao kipindi cha kiangazi mwaka jana.
Danielle Semaan, 38, na Elie wameshatalikiana, kama ambavyo anasema kwamba baada ya kuona picha za mkewe na Cesc, akaona ni bora aachane na mkewe huyo.

Wanandoa hao wawili wana watoto wawili, mtoto wa kiume mwenye miaka 11 na wa kike mwenye miaka 8.

Eli Taktouk(kushoto), akiwa na rafiki yake.

No comments: