Ombi la uhamisho wa usajili wa mkopo nje ya dirisha la
usajili la Didier Drogba limekataliwa na FIFA.
Gwiji huyo wa zamani wa The Blues amekuwa akihusishwa
na kurudi Chelsea kwa uhamisho wa mkopo wa muda
mfupi wakati wa mapumziko ya
ligi kuu ya China lakini
FIFA leo wamekataa maombi ya nahodha huyo wa Ivory
Coast.
Shirikisho hilo la soka duniani lilisema kwenye taarifa
yake: "Tunathibitisha kwamba tulipokea maombi ya
mchezaji Didier Drogba kuomba
ruhusa ya kusajiliwa nje
ya kipindi cha usajili kwa mkopo.
"FIFA imemualifu mchezaji juu ya kanuni
zilizopo.....kwamba wachezaji wanaweza kusajiliwa katika
vipindi viwili tu vya
mwaka vya usajili vilivyowekwa na
vyama vya soka."
FIFA ilisema ingewezekana tu kwa Drogba kuhama kama
asingekuwa na mkataba na kalbu nyingine ndio angeweza
kusajiliwa kwa wakati ulio
nje ya dirisha la usajili.
Drogba alikuwa anahitaji kupata sehemu ya kuendelea
kujifua kabla ya kwenda kwenye michuano ya mataifa huru
ya Afrika 2013.
|
No comments:
Post a Comment