 |
Robin van Persie alikataa ofa nzito
ambayo inakadiriwa kufikia £300,000 kwa wiki utoka kwa Manchester City
kabla hajaamua kujiunga na mahasimu wao Manchester United, hiyo ni kwa
mujibu wa kocha Arsene Wenger. Van
Persie ameendeleza makali yake ambayo msimu uliopita yalimfanya afunge
mabao 37 akiwa na Arsenal na sasa akiwa na United tayari ameshatupia
mabao tisa katika mechi 12.
Lakini magoli hayo yangeweza kuwa kwa
ajili ya timu inayovaa jezi za blue kutoka jiji la Manchester badala ya
United, baada ya Mholanzi huyo kukataa kujiunga na City, ingawa Wenger
amegoma kutaja sababu iliyomfanya RVP aitose City.
Kwa hakika zaidi inaonekana haikuwa kwasababu ya masula ya fedha, kwa kuwa City walitoa ofa ya mshahara wa £300,000 kwa wiki. Van
Persie hapati kiasi hicho pale Old Trafford, ingawa hiyo ndio fedha
ambayo inatajwa Wayne Rooney amekuwa akilipwa -ingawa United wamekanusha
hilo.
'Ni kweli Manchester City walikuwa
wakimtaka Van Persie na akaamua kuchagua kujiunga na United," alisema
Wenger akiongea na gazeti la Independent.
'Hakunipa sababu za kuikataa City lakini na mie sikutaka kujua zaidi kuhusu hilo. 'Je inaniumiza kumuona akiondoka hapa na kwenda kwenye klabu nyingine ya hapa Uingereza? Kwa kweli hilo sio jambo nililotaka! 'Ninatumaini mapokezi yake atakapocheza
nasi hayatokuwa mabaya kwa sababu ameichezea klabu yetu kwa miaka nane.
Ningependa aheshimiwe.
|

'Unadhani nashangazwa na mafanikio
anayoyapta pale United? Hapana, pale Manchester anazungukwa na wachezaji
wazuri, na Robin na hatari mno ndani ya box." - Wenger
No comments:
Post a Comment