Bondia wa Uingereza David Price amesema angelipenda kuzichapa na Dereck Chisora baada ya pambano dhidi ya Matt Skelton.
Kabla ya pambano la Price na Skelton usiku wa
Ijumaa mjini Liverpool, Price alisema ana matumaini kwamba Dereck
Chisora ataweza kuipata tena leseni yake ya ndondi kupigana nchini
Uingereza, ili waweze kuchapana katika ngumi za uzani wa heavy.
Chisora,
mwenye umri wa miaka 28, alipokonywa leseni na bodi inayosimamia ngumi
nchini Uingereza, kutokana na utovu wa nidhamu mjini Munich, Ujerumani,
katika fujo zilizotokea kati yake na mabondia Vitali Klitschko na David
Haye.
"Nadhani ni wazi kwamba ni yeye ninapaswa
kupambana naye katika kuutetea ubingwa wangu wa Uingereza, kwani nadhani
Dereck ataweza kupigana kwa kiwango kinachostahili cha hadhi ya
Uingereza," alisema Price.
Price, mwenye umri wa miaka 29, na ambaye
alikuwa atetee mikanda yake ya ubingwa wa Uingereza na Jumuiya ya Madola
usiku wa kuamkia Jumamosi mjini Liverpool, amesema hana la kuchagua
baada ya kuchapana na Skelton.
"David Haye aliwahi kuwa bingwa wa dunia, na
anatamani pambano moja tu, na tunalifahamu [Vitali Klitschko] na Dereck
Chisora atapigana kuwania taji la Uingereza, ninaamini hivyo," alisema
Price.
Price alipopigana mara ya mwisho mjini
Liverpool, kabla ya pambano na Skelton, alimshinda Audley Harrison, kwa
kumzima mara moja, kwani pambano lilisimamishwa katika raundi ya kwanza.
|
No comments:
Post a Comment