MASHABIKI wa soka nchini walitoka
mikoani kuja Dar es Salaam ili kumwona nyota wa Cameroon, Samuel Eto'o
timu yake ilipocheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars Uwanja wa Taifa,
Jumatano iliyopita.
Lakini hakuja na timu yake ikalala bao 1-0.
Benchi la ufundi la Cameroon likadanganya Watanzania kwamba straika huyo
alikuwa majeruhi. Kumbe ni uongo.
Sasa yeye mwenyewe ameibuka na kutamka kuwa aligoma kuja nchini kutokana na kuhofia kuuawa.
Nahodha huyo ameibua mjadala mzito baada ya kuwatuhumu maofisa wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT) kwa kutaka kumuua.
Sambamba
na kauli hiyo, Eto'o, amesema kwamba yuko tayari kwa mjadala wa suala
hilo ambao utarushwa moja kwa moja kupitia televisheni ya taifa.
Wanataka
kuniua, katika timu ya taifa naishi na mashushushu, si kwamba siko
makini katika hilo kwani hata jezi ya timu ya taifa navaa yangu binafsi
niliyotengenezewa na Puma, alisema mchezaji huyo kupitia Jarida la Je
Wanda.
Etoo ambaye kwa
sasa anachezea klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi pia alisema kwamba
hata anapokuwa mazoezini wakati wote yuko makini na maisha yake.
Etoo
ni miongoni mwa wachezaji 11 wa Cameroon ambao hawakuitikia wito wa
kuichezea timu hiyo mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania iliyopigwa
Jumatano iliyopita na Cameroon kulala bao 1-0 lililofungwa na Mbwana
Samatta.
Hawa wazee wametafuna fedha zetu
kiasi cha kutosha, badala ya kusimamia soka kwa ajili ya umma wako
katika mipango ya uongo, kusafiri daraja la kwanza kwenye ndege na
kunufaisha akaunti zao za siri katika mabenki ya Ulaya, alisema.
Cameroon
itaumana na Togo mwezi ujao katika mechi ya awali ya fainali za Kombe
la Dunia za mwaka 2014 na Etoo anadhani timu hiyo haina uwezo wa
kuifunga Togo.
FECAFOOT
haijasema lolote kuhusu hoja hizo za Etoo ingawa mmoja wa maofisa wa
shirikisho hilo anadaiwa kumwambia Etoo kuwa amekosa uzalendo na hoja
zake ni kichekesho.
Kocha
wa Cameroon, Jean Paul Akono, alisema jijini Dar es Salaam kwamba
anataka kupunguza wachezaji wenye umri na majina makubwa kwenye kikosi
hicho na kutengeneza kizazi kipya kitakachorejesha heshima ya Taifa hilo kisoka.
SOURCE: MWANASPOTI |
No comments:
Post a Comment