Shirikisho la
soka la Nigeria limesema leo Jumanne kwamba Kocha wa timu ya taifa
Stephen Keshi amebadili uamuzi wake wa kujiuzulu na mazungumzo baina yao
na kocha huyo yanaendelea baada ya kocha huyo kuiwezesha Nigeria
kushinda ubingwa wa Afrika.
Keshi na Super Eagles, ambayo waliifunga Burkina Faso 1-0 Sunday na
kushinda AFCON 2013, wanatarajiwa kuwasili Nigeria leo huku wakiwa
wameandalia sherehe na raisi wa nchi huko mjini Abuja.
Kujiuzulu
kwa Keshi, amabye alitangaza uamuzi wake jana kupitia radio moja huko
South Africa, kumeleta aibu kwa utawala wa soka wa nchi hiyo, ambayo
imekuwa kiandamwa na skendo za rushwa na utawala mbovu kwa miaka kadhaa
sasa.
Shirikisho hilo lilitoa taarifa leo asubuhi kuhusu kujiuzulu kwa Keshi, na kusema kwamba kocha huyo amebadilisha uamuzi wake.
Keshi alisema
jana kwamba ameamua kujiuzulu kwake kumekuja kutokana na maofisa wa NFA
kumtishia kumfukuza kazi kabla ya mechi ya robo fainali dhidi ya Ivory
Coast.
|
No comments:
Post a Comment