Kocha wa Paris St Germain Mtaliano Carlo Ancelotti ametajwa kuwa
mbioni kurithi nafasi itakayoachwa wazi na Jose Mourinho kama kocha wa
Real Madrid. Ancelotti inasemekana kuwa tayari ameingia kwenye
makubaliano yasiyo rasmi na klabu hiyo ya nchini Hispania na atachukua
nafasi hiyo siku chache baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Moja ya tetesi ambazo zimejaza kurasa za magazeti yenye habari za
michezo kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ni ile inayohusu Jose
Mourinho kuondoka kwenye klabu ya Real Madrid ambako amekuwa hana
mahusiano mazuri na baadhi ya watu akiwemo nahodha Iker Cassilas na
baadhi ya viongozi.
Carlo Ancelotti kwa upande wake amekuwa akihusishwa na taarifa za
kufukuzwa kazi na mabosi wa Paris St Germain ambao wamekuwa
hawafurahishwi na aina ya soka linalochezwa na klabu hiyo pamoja na
usajili mkubwa ambao imeufanya .
Uongozi wa Real Madrid unaamii kuwa Ancelotti ana uzoefu nauwezo wa
kuiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ulaya kama alivyowahi kufanya
mara mbili akiwa na Ac Milan pamoja na Juventus ambayo aliiongoza kufika
fainali ya michuano hiyo.
Endapo Real Madrid itatolewa kwenye hatua ya nusu fainali a ligi ya
mabingwa ambako iko nyuma kwa mabao manne baada ya mchezo wa kwanza
mwisho wa Jose Mourinho utakuwa umekaribia kwani atakuwa ameshindwa
kuipa klabu hiyo mafanikio iliyotarajia Ya kutwaa ubingwa wa ulaya kwa
mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 11 |
No comments:
Post a Comment