Mashabiki wa timu za West Ham
United na Manchester City kwa kushirikiana na uongozi wa timu zote mbili
watafanya ishara ya kumkumbuka mchezaji wa zamani aliyewahi kuzichezea
klabu zote mbili na timu ya taifa ya Cameroon Marehemu Marc Vivien Foe .
Mchezaji huyo aliyefariki dunia
uwanjani wakati akiichezea timu yake ya taifa katika mchezo dhidi ya
Colombia kwenye michuano ya kombe la mabara mwaka 2003, aliwahi
kuzichezea West Ham na Manchester City katika miaka ya 2000 na kwenye
timu zote mbili alikuwa akipendwa na mashabiki kutokana na jinsi
alivyokuwa akicheza kwa moyo na ujasiri mkubwa.
Ishara hiyo itafanywa kwenye
dakika ya 23 ya mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Etihad ambapo
mashabiki wa timu zote watasimama na kupiga makofi kwa dakika nzima.
Foe atabaki kwenye historia ya
Man City daima baada ya kufunga bao la mwisho kwenye uwanja wa zamani wa
City wa Maine Road kabla ya uwanja huo kubomolewa, alifariki dunia
baada ya kuanguka uwanjani ambapo madaktari waliomfanyia vipimo
waligundua ugonjwa wa moyo ambao ni wa kurithi ndio ulikua chanzo cha
kifo chake.
|
No comments:
Post a Comment