| Ni mtaalam wa zamani wa mambo ya
uwekezaji kwenye benki na mtu muhimu nyuma ya uongozi wa familia ya
Glazer, ndio yupo nyuma ya mafanikio ya kibiashara ya Manchester United.
Wakati Ed Woodward, 40, anaweza asiwe na jina kubwa, ameweza kujenga sifa wakati wa miaka yake nane ndani ya Old Trafford. Na kipindi kijacho cha kiangazi Woodward atachukua nafasi ya ofisa mkuu wa Manchester United David Gill mbaye atastaafu.
Akiwa amehusika kwa
kiasi kikubwa katika kuhakikisha familia ya Glazer inainunua klabu hiyo
mwaka 2005, Woodward amekuwa mtu muhimu ndani ya klabu hiyo tangu wakati
huo.
Akiwa kama msaidizi wa
Gill, muingereza huyo amekuwa na jukumu la kuhakikisha mbinu za biashara
za United zinakuwa bora, baada ya kuondoka kwa Gill 30 June, ataingia
katika majukumu ya kisoka zaidi, yakiwemo masuala ya usajili na
uhamisho pamoja majadiliano ya mishahara ya wachezaji.
|
No comments:
Post a Comment