Kocha wa Manchester United amesema hana mipango ya
kustaafu hata baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa kocha huyo
atafanyiwa upasuaji baadaye mwaka huu.
Ferguson, 71, anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kiuno Baada ya kukamilika kwa msimu huu.
Ferguson
anasema upasuaji huo hautaharibu mipango yake ya hapo baadaye na ana
matumaini makubwa kuwa ataendelea na majukumu yake kama kawaida.
Nchini Uholansi, klabu ya Ajax inasherehekea
ushindi wake wa tatu mfululizo wa ligi kuu ya premier, baada ya kuilaza
Willem Tilburg kwa magoli matano kwa yai.
Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kuwa na alama
nne zaidi kuliko wapinzani wao wa karibu PSV Eindhoven huku ikiwa
imesalia mechi moja tu kabla ya kukamilika kwa ligi kuu ya premier
nchini Uholansi.
Na klabu ya Juventus imeshinda kombe la ligi kuu ya serie A, ya Italia baada ya kuilaza Palemo kwa bao moja kwa bila hii leo.
Arturo Vidal aliifungia Juventua bao hilo muhimu
na la ushindi kunako dakika ya hamsini na tisa kupitia mkwaju wa
penalti na kuiweka juventus alama 14 mbele ya mahasimu wao wa karibu
Napoli |
No comments:
Post a Comment