Klabu ya Barcelona, imekubali kumsajili mshambuliaji matata kutoka Brazil Neymar kutoka kwa klabu ya Santos.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kukamilisha uasajili huo siku ya Jumatatu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Barcelona, vilabu hivyo viwili vimeafikiana kuhusu usajili wa mchezaji huyo.
Barcelona imemtaja mshambuliaji huyo kama mchezaji ambaye ana uwezo wa kuwa bora zaidi duniani.
Katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram,
Neymar, alichapisha ripoti kuthibitisha usajili huo na kuwashukuru
mashabiki wa Santos, kwa kumuunga mkono katika kipindi cha miaka tisa
iliyopita.
Katika taarifa hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kireno, Neymar, alisema licha ya kuondoka daima moyo wake utasilia na klabu hiyo.
Awali kulikuwa na fununu kuwa klabu ya Real
Madrid, vile vile ilikuwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo ambaye
mkataba wake na Santos ungemalizika msimu ujao.
Neymar atachecheza mechi yake ya mwisho siku ya
Jumapili dhidi ya Flamengo, kabla ya kujiunga na Bercelona baada ya
fainali za kombe la Shirikisho, ambayo itachezwa kuanzia tarehe kumi na
tano hadi thelathini mwezi ujao nchini Brazil.
Katika habari zingine, mshambuliaji matata wa
Manchester City Sergio Aquero, amesaini mkataba mpya ambao utaongeza
muda wake kwa mwaka mmoja zaidi.
Mchezaji huyo kutoka Argentina ambaye alisaini
mkataba wa miaka mitano mwaka wa 2011, kutoka kwa klabu ya Atletico
Madrid sasa atasalia na Manchester City hadi mwaka wa 2017.
Aguero ndiye aliyefunga bao lililoifanya
Manchester City kunyakuwa kombe la ligi kuu mwaka uliopita wakati
walipokuwa wakichuana na QPR |
No comments:
Post a Comment