Gerardo Martino
amemwambia David Moyes kwamba Cesc Fabregas hauzwi baada ya
kutambulishwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu ya FC Barcelona kwa mkataba
wa miaka miwili.
Kocha huyo wa zamani wa
Newell's Old Boys amerithi mikoba ya Tito Vilanova, ambaye alilazimika
kujiuzulu kutokana matatizo yake ya kiafya.
Akiongea kwenye mkutano
wa waandishi wa habari leo Ijumaa, Martino alisema: 'Man United inamtaka
Cesc? Kama klabu ilikataa ofa mbili za kwanza, mie nitaikataa ya tatu.
Cesc atabaki hapa.'
Makamu wa Raisi wa Barca
Josep Maria
Bartomeu amethibitisha maneno ya Martino, akiongeza: 'Ni kawaida United
kuvutiwa na mchezaji, lakini tunamtegemea Cesc na hatutomuuza,
haijalishi watatoa ofa ya kiasi gani.'
|
No comments:
Post a Comment