PSI

PSI

Thursday, August 29, 2013

Nike yazindua Sneeker mpya ya Lebron James.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya nchini Marekani Nike hii leo aimezindua rasmi kiatu cha Mchezaji bora wa NBA Lebron James .
Kiatu hicho kinachoitwa  “NIKE LEBRON 11” kimetengenezwa maalum kwa wachezaji wa Basketball ambapo kimeundwa kitaalamu kusaidia wanapokuwa uwanjani .
Muundo wa kiatu hicho ni mwepesi kuliko kawaida kitu kinachokifanya kiwe mahsusi kwa wachezaji wa ligi ya NBA hasa pale wanapokimbia kuelekea kufunga pointi wakati wa michezo ya ligi hiyo .
Pamoja na hayo bado kina muonekano mzuri utakaowavutia wale wanaopenda ‘mikato’ au swag za kileo wanapokuwa wanatoka huku wamekivaa.

Nike wamekuwa wakifanya vizuri kwenye soko la viatu vya mpira wa kikapu ambapo kiatu chenye nembo ya Lebron James kiliongoza kwa mauzo kwa mwaka uliopita ambapo kiliuza dola milioni mia tatu .
Kiatu hicho kitaingia sokoni rasmi mwezi oktoba tarehe moja huko nchini China kabla ya kuingia nchini Marekani Oktoba 12 na sehemu nyingine dunia baada ya hapo.

No comments: