Chelsea
inakaribia kumsajili mshambuliaji Samuel Eto’o kwa dili la mwaka mmoja
lenye thamani ya £7million kwa mkataba wa mwaka mmoja leo Alhamisi baada
ya kukiri kushindwa kumpata mshambuliaji wa Manchester United Wayne
Rooney.
Eto’o, 32, amekubali kupunguza dau lake alilokuwa akilipwa na Anzhi kiasi cha £17m kwa mwaka na sasa atasaini atasaini akiwa huru.
Pamoja na
hilo, lakini inaeleweka kwamba Anzhi wamemlipa Eto'o millioni kadhaa ili
kuweza kumuondoa katika listi wachezaji wanaolipwa fedha nyingi ndaniya
klabu ya Anzhi.
Eto'o aliwasili jijini London jana usiku na anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea
Cobham. |
No comments:
Post a Comment