Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ambaye hivi karibuni alipewa
zawadi ya kiwanja na Rais Jakaya Kikwete baada ya ushindi wake dhidi ya
bondia wa Marekani, ameamua kurudi shule.Cheka anasema hakupata nafasi
ya kwenda shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la
saba. “Mimi sikusoma niliishia darasa la saba, lakini nimeamua kurejea
darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph”.
“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo
hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee
na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine “.Habari kamili ipo kwenye
gazeti la Mwananchi la Sept 17. |
No comments:
Post a Comment