Wakati mshambuliaji Lomeu Lukaku akiota kurudi kuichezea Chelsea
iliyompeleka kwa mkopo Everton,kocha wa the blues Jose Mourinho
amepigilia msumari mzito akithibitisha kuwa hakuna uwezekano wa
mshambuliaji huyo kurudi darajani msimu huu.
Mourinho anasema mshambuliaji huyo ataendelea kubaki huko Goodison Park mpaka mwisho wa msimu mwezi May.
Mourinho anasema mshambuliaji huyo ataendelea kubaki huko Goodison Park mpaka mwisho wa msimu mwezi May.
Lakini kocha huyo akasema Lukaku ni mzuri Everton na kama ataendelea
kucheza kila mchezo itamjengea mazingira mazuri ya baadaye kwa Chelsea.
Wikiendi Lukaku aliisaidia Everton kuichapa West Ham baada ya kutupia bao la ushindi katika mchezo ambao ulikuwa na misukosuko kwake baada ya kuumia wakati anafunga na akisema hata hakufahamu kama ni yeye ndiye kafunga hilo goli.

Chelsea kwasasa katika safu ya ushambuliaji wana Samuel Etoo,Fernando Torres na Demba Ba wanaogombea namba.

No comments:
Post a Comment