Mshambuliaji mwenye miaka 20 Stephan
El Shaarawy anataka kuondoka AC Milan kwenda kusaka maisha mapya
yatakayomfanya kupata nafasi ya kucheza.Maamuzi
hayo yanawafanya Chelsea, Tottenham na Arsenal kuingia vitani lakini
Liverpool inaelezwa ndio wana nafasi kubwa zaidi ya kuzizidi kete klabu
hizo.El
Shaarawy alifunga mabao 16 msimu uliopita lakini sasa Mario Balotelli
ndio anaonekana kuchukua nafasi zaidi kwenye klabu hiyo huko San Siro.Wamiliki wa Liverpool wanapanga mipango ya kununua wachezaji wadogo na El Shaarawy anaonekana kufit kwenye mipango hiyo.Mshambuliaji huyo anakadiriwa kufikia dau la paundi milioni 25.
No comments:
Post a Comment