Arsenal yaifumua Liverpool 2 - 0
Arsenal imeilaza Liverpool kwa
jumla ya magoli 2 - 0 katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa
siku ya Jumamosi katika uwanja wa Emirates jijini London.
Arsenal walianza kuandika goli la kwa kwanza
lilofungwa na Santiago Cazorla katika dakika ya 19 kipindi cha kwanza
baada ya kipa wa Liverpool Simon Mignolet kuutema mpira na kurudi
uwanjani.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Arsenal walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa goli 1 - 0.
Kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani na
kuanza kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika ya 59 Aaron Ramsey
alinogesha sherehe ya Arsenal kwa kupachika goli pili.
Kwa matokeo hayo Arsenal sasa itakuwa
imejiimarisha kileleni mwa msimamo ligi kuu ya England kwa kujikusanyia
jumla ya pointi 25.
No comments:
Post a Comment