PSI

PSI

Saturday, November 30, 2013

CS Sfaxien mabingwa Shirikisho Afrika

Pamoja na kufungwa ugenini magoli 2 - 1 na TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Club Sportif Sfaxien ya Tunisia imenyakua kombe la shirikisho barani Afrika kufuatia kushinda mechi ya mkondo wa awali kwa jumla ya magoli 2 - 0.
Kwa matokeo hayo CS Sfaxien iimeiadhibu timu ya TP Mazembe kwa jumla ya magoli 3 - 2.
Mechi hiyo ya fainali mkondo wa pili imechezwa kwenye uwanja wa Lubumbashi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
CS Sfaxieni wananyachukua kombe hilo kwa mara ya tatu baada ya kulinyakua mwaka 2007 na 2008 . TP Mazembe ilikuwa ikijaribu kunyakua kombe hilo kwa mara ya kwanza lakini ndoto hizo zimezimwa Club Sportif Sfaxien ya Tunisia .
TP Mazembe pamoja na kushindwa kunyakua kombe hilo la shirikisho barani Afrika, imeshanyakua kombe la Klabu Bingwa bara Afrika kwa mara kadhaa.
Mshindi wa kombe hilo Club Sportif Sfaxien ya Tunisia pamoja na kunyakua kombe hilo pia klabu hiyo imepewa kitita cha dola za kimerekani 660,000 ambazo ni zawadi kwa bingwa wa kombe hilo.
Vile vile CS Sfaxien itakutana na Klabu Bingwa barani Afrika Ahly ya Misri mwaka kesho katika kombe la maalum la "CAF CAF Super Cup"

No comments: