PSI

PSI

Monday, November 4, 2013

Mourinho ruksa kusajili mshambuliaji January,Torres,Etoó,Demba wakalia kuti kavu


Kocha Jose Mourinho amewashiwa taa za kijani kusaini mshambuliaji mpya wakati wa usajili wa dirisha dogo mwezi January ili kuendelea na changamoto ya kuusaka ubingwa.

Mourinho binafsi anachanganywa na mshambuliaji Fernando Torres aliyesajiliwa kwa dau la paundi milioni 50 na Samuel Eto'o kufunga goli moja katika ligi kuu ya England huku Demba Ba,mshambuliaji chaguo la tatu kutofunga bao mpaka sasa tokea alipofunga dhidi ya West Bromwich March 2.

Chelsea wapo pointi tano nyuma ya vinara Arsenal baada ya kukubgali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Newcastle,lakini Mourinho tayari ameamua kufanya mabadiliko kwenye safu ya ushambuliaji.

No comments: