PSI

PSI

Saturday, December 28, 2013

Chelsea kumtoa sadaka Demba Ba

 

Chelsea wako tayari kumtoa sadaka mshambuliaji wake Demba Ba ili kumnasa Fredy Guarin kutoka Inter Milan ya Italia.

The Blues wako tayari kukaa na Inter Milan ili kumnasa kinda huyo wakati wa usajili wa dirisha dogo katika harakati za kutaka kujiimarisha hasa katika safu ya ushambuliaji inayoonekana kutokaa sawa.

Inaelezwa kuwa inaweza kuwaghalimu Chelsea kitita cha paundi milioni 16 ili kumnasa kinda huyo wa Colombia ambaye amewahi kucheza FC Porto.

Walter Mazzarri bosi wa Inter Milan hata hivyo ana shaka kama Ba ataweza kuwa mtu sahihi kwenye kikosi chake.

No comments: