Adebayor akiwa na kocha wake baada ya kufunga bao
Emmanuel Adebayor kwa mara
nyingine tena alifunga magoli mawili na kudumisha harakati za Tottenham
za kusalia katika nafasi nne bora kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier.
Tottenham waliilaza Necastle kwa magoli manne bila jibu.
Adebayor
alifunga bao la kwanza kunako dakika ya kumi na tisa baada ya kipa wa
Newcastle Tim Krul kutema mkwaju uliopigwa na Nabil Bentaleb.
Adebayor vile vile alichangia bao la pili wakati
Krul kwa mara nyingine alipoutema mkwaju wake na kuumpa nafasi Paulinho
kumalizia na kufunga la pili.
Nacer Chadli naye aliandikisha jina lake
miongoni mwa wachezaji waliofunga goli mwaka huu pale alipofunga bao la
tatu, baada ya kuvurumisha kombora kali kutoka umbali ya mita ishirini
hivi.
Juhudi za Newcastle ziliambulia patupi pale kipa
wa Spurs Hugo Lloris alipookoa mikwaju iliyopigwa na Papiss Cisse,
Mathieu Debuchy na Yoan Gouffran.
Newcastle sasa haijafunga bao lolote katika
mechi saba kati ya nane zilizopita na pia kuandikisha rekodi ya kupoteza
mechi nne mfululizo katika uwanja wao wa nyumbani kwa mara ya kwanza
tangu mwaka wa 1987.
Adebayor akiwa na kocha wake baada ya kufunga bao
No comments:
Post a Comment