Kiwanja Qatar 2022
Kamati andalizi ya kombe la
dunia mwaka wa 2022 itakayoandaliwa huko Qatar imetoa mustakabali mpya
utakaosimamia uhusiano baina ya wenye kandarasi na wafanyikazi wa kigeni
wanaojenga viwanja vitakavyotumika katika michezo hiyo.
Takriban wajenzi 200 raiya wa Nepal waliripotiwa kufariki katika miradi ya ujenzi mwaka uliopita.
Kulingana na Shirika la
International Trade Union iwapo hali itasalia ilivyo sasa nchini Qatar
wafanyi kazi takriban 4000 watakuwa wamepoteza maisha yao katika ujenzi
wa viwanja na muundo msingi wa kombe hilo la dunia.
Taifa hilo la Ghuba lilikuwa na makataa ya hadi
tarehe 12 Februari 2014 kuifahamisha shirikisho la soka duniani Fifa
mikakati ya kuboresha hali ya utendakazi wa wafanyikazi .
Mustakabali huo mpya wa utendakazi wenye ukurasa 50 ,umeundwa kwa ushirikiano wa shirika la wafanyikazi duniani ILO.
Mbali na vifo vya wafanyikazi 185 mwaka
uliopita,inaaminika kuwa idadi kubwa ya wafanyikazi wamejeruhiwa kazini
kutokana na mazingara mabaya ya kufanyia kazi.
Kumeibuka ,pia maswali kuhusiana na makazi duni ya wafanyikazi.
Kumeibuka ,pia maswali kuhusiana na makazi duni ya wafanyikazi.
Mashirika ya wafanyikazi na yale ya kupigania
haki za kibinadamu yamelalamikia vikali mfumo wa Qatar wa uajiri uitwao
''Kefala '' ambao unapatanisha hati ya usafiri ama VISA na kampuni
inayowaajiri mfanyikazi.
Wafanyakazi Qatar 2022
Mashirika hayo yanasema kuwa mfumo huo
unawanyima wafanyikazi haki ya kuondoka Qatar bila ya idhini ya mwajiri
wao pindi wanapotofautiana ama kudhulumiwa.
Katibu Mkuu wa kamati andalizi ya qatar 2022
Hassan Al-Thawadi, amesisitiza kuwa mashindano hayo hayatafaidi jasho na
damu ya watu.
Hali na haki ya wafanyikazi wanaojenga viwanja
vya kombe la dunia vitakavyotumika mwaka wa 2022 ilizua mjadala mwaka
uliopita baada ya mashirika ya kupigania haki za wafanyikazi duniani
kudai kuwa wenye kandarasi za kujenga viwanja na muundo msingi wa Qatar
2022 walikuwa wamewaajiri raiya wa kigeni ambao walikuwa wanafanyishwa
kazi bila malipo ama kwa malipo duni.
Qatar2022Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp
Blatter aliingilia kati na kuahidi kufanya mashauriano na Kiongozi wa
taifa hilo lenya utajiri mkubwa wa mafuta.
Mashindano hayo yameripotiwa kuwa yataigharimu Qatar dola bilioni 200
No comments:
Post a Comment