Mashabiki wamtaka Wenger aondoke
Arsene Wenger aendelee au asiendelee?
Ndio wimbo unaorindima ndani ya mioyo ya mashabiki wa Arsenal.
Hii ni baada ya kuchapwa 3 na Everton jana.
Mashabiki wanamlaumu Wenger naye Wenger mwenyewe anakilaumu kikosi chake.
"Lililobaki kwa silimia 100 tutang'ang'ania nafasi ya nne ingawaje ni vigumu," Wenger amesema.
Ratiba ya Arsenal
- Tue 15 April: v West Ham (H)
- Sat 19 April: v Hull (A)
- Mon 28 April: v Newcastle (H)
- Sat 3 May: v West Brom (H)
- Sat 11 May: v Norwich (A)
Wenger ambaye amehudumu katika wadhfa huo katika
mechi 1003 amewahi kuingoza timu hiyo ya Uingereza kufuzu kwa
mashindano 16 ya kombe la mabingwa barani Ulaya.
Shabiki mmoja auliza katika mtandao wa twitter
kuwa iweje January walikuwa nambari moja, february nambari 2, Mwezi wa
tatu 3 na sasa mwezi wa nne nambari nne?
Mashabiki wamtaka wenger ajiuzulu
Mwingine asema Bwana Wenger amemtetea kwa miaka mingi - tisa kwa idadi -lakini leo amekoma.
Amejiunga na wale ambao wameanzisha kampeni katika mtandao Wenger ajiuzulu.
Kilio cha Arsenal ni furaha ya Liverpool ambao baada ya kuitandika West ham 2-1 wametuliza kileleni mwa ligi
Bashasha sasa pia zasikika katika kambi
iliyokuwa imefifia ya Manchester United baada ya kuimwagia machungu yao
yote Newcastle 4- 0 .
Kutokana na Ushindi huo Vijana wa David Moyes hatimaye wameimarika kutoka nafasi ya 7 hadi nambari 6
No comments:
Post a Comment