Kama mwanaume ambaye hapendi kukubali
kuwa wa pili kwa ubora, Sir Alex Ferguson lazima atakuwa akiudhiwa sana
na namna jinsi amekuwa akiwakosa wachezaji anaotaka kuwasajili hasa
kwenye miaka ya karibuni kabla ya kugeukia kwa wachezaji wa plan B.
Mchezaji
mpya kuongezeka kwenye listi ya ambao Fergie amewataka lakini akawakosa
ni Luka Modric, ambaye Sir Alex amekuwa akimuwania kwa miaka sasa na
alitaka kumsaini ndani ya klabu yake ya Manchester United kwa misimu
miwili iliyopita.
Katika mara mbili zote, kikwazo kikubwa
kimekuwa ni bei ambayo Tottenhma Hotspur wamekuwa wakiitaka £40million
kwa Croatia huyo na United kugoma kulipa au kushindwa kumudu bei ambayo
inapingana na sera zao za usajili.
Modric angekuwa mtu sahihi
kwenye kikosi cha United. Mrithi halisia wa Paul Scholes ambaye anaweza
kuimudu nafasi ya kiungo wakati, mchezaji huyo wa zamani wa Dinamo
Zagreb sasa kuna uwezekanao mkubwa akajiunga na Real Madrid, huku
kuondoka kwake White Hart Lane kukionekana hakuzuiliki.
Hali hii
imekuwa ya kawaida kwa United tangu kuwasili kwa kwa wamiliki wapya wa
klabu hiyo mwaka 2005. Wakati mabingwa hao wa mara 19 wa soka la England
wakiwa na historia kubwa na ubora wa kikosi chao, mikataba ya mamilioni
ikiendelea kumiminika na umaarufu ukizidi kukua miongoni mwa mashabiki
wa soka duniani.
Ferguson alitumaini jambo hili lingebadilika
msimu huu, lakini kuchelewa kwa mipango ya wamiliki wa klabu kuingia
kwenye soko la hisa la Singapore kumewafanya United kukosa fedha nyingi
za kupambana kwenye soko la usajili.
Ferguson amekuwa akiongea
juu ya kukosekana kwa thamani ya ukweli kwenye soko la usajili, lakini
mashabiki wa United wanakumbuka wakati Mscotland huyo alivyokuwa
akifurahia kuvunja rekodi za usajili wakati alipokuwa akiwanunua akina
Jaap Stam, Juan Sebastian Veron na Rio Ferdinand.
Dimitar
Berbatov, alisajilia kutoka Spurs kwa ada ya £30.75million mwaka 2008,
labda ndio pekee ambaye tunaweza kumtoa kwenye listi kwa kuwemo ndani ya
kipindi cha utawala wa Glazers lakini United hawakuwa na upinzani
mkubwa kwa ajili saini yake na mahitaji yake binafsi ya mshahara
yalifikia sera ya usajili na bajeti ya Manchester United.
Hilo
hilo haliwezi kusemwa kwa Eden Hazard, mbelgiji ambaye alikata United na
majirani zao City na kusajili Chelsea mwezi uliopita.
United
walihisi wapo kwenye nafasi nzuri ya kumsaini Hazard kutoka Lille,
lakini hawakuwa radhi kumlipa mchezaji zaidi ya £130,000 kwa wiki
achilia mbali fedha ya wakala wake £6million.
Chelsea wakawazidi
United kwa kutoa ofa ya £200,000 kwa wiki na kukubali kulipa fedha za
wakala, wakawalazimisha United kumgeukia mchezaji aliyekuwa kwenye plan B
na wakamsajili Shinji Kagawa kutoka Borussia Dortmund.
Kiangazi
kilichopita, United walishindwa tena na mahasimu wao Manchester City
katika mbio za kumsaini Samir Nasri kutoka Arsenal kwa kushindwa kutoa
ofa ya mkataba wa £170,000 kwa wiki. Wesley Sneijder, target mwingine wa
usajili, alikataa kukubali kushusha mahitaji yake ya kupata mshahara wa
£200,000 na akabaki Inter Milan.
Mara nyingine zimekuwa sababu
za kisoka kwa United kuwakosa wachezaji wanaowataka. Ferguson alikuwa
akimuimbisha Karim Benzema kwa takribani miaka miwili lakini
mshambuliaji huyo wa kifaransa alikuwa ameweka nia ya kuichezea Real
Madrid, wakati David Villa alikuwa hayupo radhi kuondoka Spain na
akasaini kuichezea Barelona akitokea Valencia mwaka 2010.
Lakini
wachezaji hawa wa hadhi ya juu - miongoni mwa walio bora duniani kwenye
nafasi zao ndio ambao United wanahitaji kama ikiwa wanataka kuurudisha
ubingwa wa England kwenye kabati la makombe pale Old Trafford na kuweza
kutoa ushindani kwenye michuano ya Ulaya.
Ni vipi Ferguson
anaweza kuongelea bei kubwa za wachezaji wakati yeye ni mmoja ya watu
waliochangia hilo hasa ukizingatia alimuuza Cristiano Ronaldo kwa bei
£80million cash kwenda Real Madrid 2009? Hi ni bei ambayo kwa wakati ule
angeweza kuinunua klabu nzima ya Newcastle.
Fergie anajua vizuri
thamani ya wachezaji wa kisasa kwenye soko la usajili - na anajua
kwamba hana fedha za kuwasajili kulingana na bajeti anayopangia na
mabosi wake.
United wana deni linalokaribia £500million pamoja na
riba yanaizuia klabu hiyo kwenye kushindana kwa fedha na klabu kama
City, Chelsea na mabwana wawili wa ligi ya Spain.
Manchester
United hawahitaji sugar daddy kama ilivyo kwa Chelsea na City - mapato
yao ni hatari, ni fedha nyingi sana - lakini deni kubwa walilonalo
wamiliki linaikabaka klabu hiyo shingoni. Na ukweli bila kupata
uwekezaji mkubwa kuna hatari City watawapa taabu sana na hata kuwashinda
kama klabu inayoongoza England kwenye miaka kadhaa ijayo mbeleni.
|
No comments:
Post a Comment