PSI

PSI

Thursday, June 28, 2012

OFFICIAL: JORDI AITOSA MAN UNITED - KUJIUNGA NA BARCELONA WIKI IJAYO

Barcelona wametangaza kwenye mtandao wao rasmi kwamba wamekubalina na Valencia juu ya ada ya uhamisho wa mchezaji wa kimataifa wa Spain Jordi Alba.

Barca ambao wamekuwa wakihusishwa na beki huyo wa kushoto kwa muda mrefu sasa, wamepiga hatua kubwa kuelekea kukamilisha dili hilo lenye thamani ya ‹€14 million.

Alba atakwenda Barcelona kufanya vipimo wiki ijayo, na kusaini dili la mkataba wa miaka 5 mara tu atakapofaulu vipimo vya afya.

"Barcelona wametangaza kwamba makubaliano rasmi yamefikiwa juu ya ada ya uhamisho wa Jordi Alba, kilichobaki ni vipimo vya afya ambavyo mchezaji huyo atafanyiwa wiki ijayo jijini Barcelona." Uliandika mtandao huo wa Barca.

"Gharama za uhamisho huu ni €14million na mchezaji atasaini mkataba wa miaka 5."

Alba mwenye miaka 25 ni zao la chuo cha soka cha Barcelona La Masia, lakini alifeli kufanikiwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza pale Nou Camp na akaondoka mwaka 2005


No comments: