Gazeti la the Sun limeandika
line chache na nzito kuhusu maamuzi mapya ya Mchezaji ASAMOAH GYAN ambae
amekamilisha uhamisho wake wa moja kwa moja kutoka Sunderland kwenda
kucheza soka lake United Arab Emirates akiwa tayari amekipiga kwa mkopo
na club hiyo ya Al-Ain kuanzia msimu uliopita.
Mshkaji huyu Mghana alijiunga
na Black Cats kutokea Ufaransa kwa ada ya pound milioni 13 mwaka 2010 na
alifunga magoli 11 kwenye msimu wake wa kwanza ndani ya English
football, pamoja na kufanya uamuzi wa kwenda kucheza U.A.E amesema
anajua watu watamkosoa lakini anaifanya kazi yake, alilijadili hilo na
familia yake na ikakubali, ni maisha yake.. anachotaka ni kwenda kucheza
soka la kiwango.
|
No comments:
Post a Comment