MABINGWA watetezi wa Kombe la Kagame, Yanga leo wameanza vibaya baada ya
kufungwa bao 2-0 na wapinzani wao Atletico ya Burundi, mchezo uliopigwa katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji
wa Didie Kavumbagili katika dakika ya 80 akitumia vyema mpira vyema mpira wa
kona baada ya mabeki wa Yanga, Nadir Haroub 'Cannavro' na Kelvin Yondani
kushindwa kuokoa kabla ya kutiga wavuni.
Timu hizo dakika zote
zilishambuliana na huku kila moja ikishinshindwa ikiokoa mashambulilizi kutokana
na aina ufundi wa wachezaji hao ulionyeshwa .
Baada ta mechi hiyo Kocha
Mkuu wa Yanga, Tom Saintfiet alisema timu yake ilicheza vizuri huku akitupa
lawama kwa washambuliaji wake Jerry Tegete na Hamis Kiiza kushindwa kutumia
vyema nafasi walizokuwa wanazipata.
Saintfiet alisema, kufungwa huko
kusiwakatishe tamaa mashabiki na wapenzi wa Yanga, badala yake kukiiunga mkono
katika michezo inayofuata ili watete taji hilo wanaloshikilia ya
Kagame.
Kocha huyo, amesifu safu ya kiungo iliyoongozwa na Haruna
Niyozima na Rashidi Gumbo iliyocheza kwa kuelewana na kumiliki kiungo katika
dakika zote 90 licha ya kutopata bao .
Kwa upande wa Kocha wa Atletico,
Kazee Cerbric alisema aina ya uchezaji ya Yanga ya butua butua ndiyo iliyompa
ushindi wa bao hilo, kutokana na wachezaji wa timu hiyo kushindwa kumiliiki
mpira.
Cerbric alisema, aliingia uwanjani kwa tahadhari kubwa dhidi ya
Yanga akiamini kuwa kutokana na hasira walizonazo za kupoteza taji la Ubingwa wa
Ligi Kuu ya Tanzania Bara .
"Niliingia kwa tahadhari kubwa ya Yanga
kupoteza ubingwa nikiamini kuwa watacheza vizuri na hata kupata ushindi
wawariridhishe mashabiki wao kufuatia ubingwa huo waliukosa," alisema Cerbric
.
Mabingwa wa ligi, Simba kesho saa 10:00 jioni wanatarajia kujitupa
kwenye Uwanja wa Taifa kuvaana na URA ya Uganda mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaa.
|
No comments:
Post a Comment