VICENTE DEL BOSQUE
Real Madrid wana historia ya kubadilisha makocha wao kuliko
wanavyobadilisha vitambaa vya meza za kulia msosi kwenye canteen, lakini
kocha wa sasa wa Spain Del Bosque anaweza kuwa ndio aliyefukuzwa kwa
kuonewa kuliko wengine. Akiwa ameshinda makombe mawili ya La Liga,
mawili ya champions league, Spanish Supercup, UEFA Supercup na
Intercontinental cup wakati akiwa kiongozi wa benchi la ufundi la Los
Blancos, aliiongoza klabu kupata mafanikio makubwa katika historia ya
klabu hiyo.
Mara magalatico wakaanza kuja kwenye klabu bila ruhusa ya kocha, klabu
ikafanya uamuzi wa kushtusha zaidi ulipoamua kutomuongeza mkataba mpya
Del Bosque mwaka 2003. Matokeo yake akaondoka na klabu ikashindwa
kufanya vizuri hata kufikia kukaa misimu minne bila kombe la maana mpaka
mwaka 2007 (chini ya Fabio Capello) pamoja na kutumia mipesa mingi
katika kununua wachezaji wakubwa.
|
No comments:
Post a Comment