Tangu Mwimbaji Star Rihanna
alipoingia kwenye muziki 2006 Maisha yake ya kimapenzi yamekua gumzo
kwenye media na kwa mashabiki wa muziki wake ambapo mwimbaji huyo amemua
kuweka wazi ishu za mapenzi zinazoendelea kwenye maisha yake ya sasa.
Rihanna mwenye umri wa miaka 24
amesema amekua mkali kwenye maisha yake ya mapenzi sasa hivi na ni kama
mapenzi hayapo kwake, yani kama akikutana na mtu ambae yuko poa
ataenjoy nae lakini dakika atakayogundua kwamba wanakaribia kuingia
kwenye mapenzi, au kutakwa.. atajiondoa mara moja kwa sababu sasa hivi
hapendi kuruhusu watu waingie moyoni mwake kimapenzi tena kwa sababu
anaogopa kuumizwa.
According to Global grind, Riri
amesema wakati alipofall inlove, liumizwa sana na ni kwa sababu alikua
amependa kweli, alipoumizwa alijihisi hana thamani na maisha yake
yalibadilika, kila alichofaham kilibadilika, hakuwahi kudhani kama
angeweza kuumizwa kiasi kile na asingependa yaliyomkuta yatokee tena.
Haya maneno ya Rihanna
yameonekana kuuzungumzia uhusiano wake na mwimbaji Star Chris Brown
ambapo RiRi anaonekana pia kutopenda tena baada ya uhusiano wao
kuvunjika kwa ugomvi mkubwa. |
No comments:
Post a Comment