Ikiwa unaishi nchini Marekani na ukapenda kuwaona Real Madrid, then kuna taarifa nzuri na mbaya kwa ajili yako.
Taarifa
nzuri ni kwamba mabingwa hao wa Spain watakuwa wakifanya mazoezi kwenye
sehemu ya wazi kwa wale ambao wangependelea kuwaona: habari mbaya ni
kwamba itabidi uichimbue sana mifuko yako kuweza kulipia kuwaona Ronaldo
na wenzie wakifanya mazoezi. Gharama za tiketi kuwaona Madrid zimepanda
mpaka kufikia €311 kwa kipindi cha saa moja na nusu kuweza kumshuhudia
Mourinho akitoa maelekezo huko Los Angeles mwezi August tarehe 4.
Tiketi
ya bei rahisi itagharimu kiasi cha €69, lakini tiketi ya gharama zaidi
itakayokuwa ikihusisha kupata breakfast pamoja na kuweza kukutana na
wachezaji na kuongea nao itarudi na kufikia €311 ambayo ni sawa na kiasi
kisichopungua 650,000 za kibongo.
Na kama utapenda kuangalia mazoezi na kwenda kuangalia mechi ya kirafiki dhidi ya LA Galaxy, then itabidi uongeze €448 |
No comments:
Post a Comment