Rais wa sasa wa shirika linalotawala mpira duniani
Fifa Bw.Sepp Blatter alifahamu kuwa wakuu wenzake wanapokea mlungula,
kwa mujibu wa uchunguzi uliofichuliwa na Mahakama kuhusu ruishwa.
Aliyekuwa Rais wakati huo Joao Havelange pamoja
na mwanachama mkuu wa kamati ya utendaji Ricardo Teixeira walitajwa
jumatano katika tuhuma za kupokea mlungula kutoka kampuni
inayoshirikiana na FIFA kama mkondo wake wa biashara na masoko.ISL.
Hakuna baina yao aliyelaumiwa na FIFA wala kuonywa.
Kwenye wavuti ya Fifa, Sepp Blatter anasema kuwa
alifahamu kuhusu malipo hayo ingawa ameongezea kusema kuwa yalikua
halali wakati ule.
Blatter amesema kuwa, wakati huo, malipo ya aina
hiyo yangeweza hata kukatwa kutoka kwenye fungu la kodi kama gharama za
biashara. Kwa leo, hilo linaonekana kuwa tendo la kihalifu.
Korti moja ya Uswizi iliamuru nyaraka
zilizofichua kisa hicho na Maofisa waliohusika waliopokea mlungula
kutoka kampuni ya ISL watajwe.
Kampuni hiyo ya ISL ilifilisika mnamo mwaka 2001.
Nyaraka zilizotaja majina ya Maofisa wa Fifa
waliohusika ziliruhusiwa kuchapishwa na vyombo vya habari, ikiwa ni
pamoja na BBC, zikitowa maelezo kamili yaliyohitimishwa mnamo mwezi Mayi
mwaka 2010 |
No comments:
Post a Comment