PSI

PSI

Friday, July 13, 2012

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WAO KWA KUIFUNGA AZAM KWA PENATI

Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati,  baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa leo hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.


Wachezaji wa timu ya Simba pamoja na kocha wao wakipiga picha pamoja na kombe lao walilolikabidhiwa leo kwenye uwanja wa Taifa baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika michuano ya Urafiki inayoandaliwa visiwani Zanzibar.
Wachezaji wa timu ya Simba wakisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuchukua ubingwa wa kombe la Urafiki
Mchezaji wa kimataifa wa timu ya Simba kutoka nchini Zambia Felix Sunzu akichuana vikali na beki wa timu ya Azam FC katika mchezo huo.

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC kwenye uwanja wa Taifa.

No comments: